Fang Bin na watu wengine ambao walitajwa kama wanahabari wa kiraia walichapisha maelezo ya janga hilo mapema 2020 kwenye tovuti na mitandao ya kijamii, na kuwaaibisha maafisa wa China ambao walikabiliwa na ukosoaji kwa kushindwa kudhibiti mlipuko.
Video ya mwisho Fang, muuzaji wa nguo za kitamaduni za Kichina, iliyowekwa kwenye Twitter ilikuwa ya kipande cha karatasi kilichosomeka, “wananchi wote wanapinga, rudisha nguvu kwa watu.”
Kesi ya Fang ni sehemu ya ukandamizaji wa Beijing juu ya wakosoaji wa kushindwa kwa China kukabiliana na janga hilo mapema.