Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:14

Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yaongeza misaada ya kuokoa maisha kwa maelfu Ukraine

Jengo la jumba la mazoezi lililoharibiwa na shambulio la kombora la Russia huko Mykolaiv, Ukraine Novemba 1, 2022.REUTERS
Jengo la jumba la mazoezi lililoharibiwa na shambulio la kombora la Russia huko Mykolaiv, Ukraine Novemba 1, 2022.REUTERS

Kuelekea maadhimisho ya mwaka wa kwanza wa uvamizi wa Russia nchini Ukraine Februari 24, mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakiongeza misaada ya kuokoa maisha kwa maelfu ya watu wanaoishi katika maeneo yaliyogubikwa  na vita.

Misafara miwili ya mashirika ilifikia jamii zenye mahitaji makubwa kwenye mstari wa mbele wiki iliyopita. Msafara wa lori sita uliwasili katika mji wa Toretsk mashariki mwa Ukraine, takriban kilomita 10 kutoka eneo la mapigano katika mkoa wa Donetsk, Jumanne iliyopita.

Jens Laerke, msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu, OCHA, alisema msafara huo ulibeba misaada muhimu, ikiwa ni pamoja na maji, dawa, na vifaa vya dharura vya makazi.

Msafara huo pia ulipeleka vifaa vya dharura na vifaa vya upasuaji wa dharura, alisema. Takriban watu 15,000 kati ya wakaazi 75,000 walioishi huko kabla ya vita bado wako katika mji huo na jamii za karibu.

Waasi wanaoiunga mkono Russia waliiteka Toretsk kwa muda mfupi baada ya vita kati ya waasi wanaoungwa mkono na Russia na serikali ya Ukraine kuzuka katika eneo la Donbas mwaka wa 2014. Na wakati vikosi vya Ukraine viliichukua tena Toretsk baadaye mwaka huo, mji huo umekuwa kwenye mapigano tangu wakati huo na usambazaji muhimu wa maji ulikatwa mara nyingi.

XS
SM
MD
LG