Wafugaji hao wa Loliondo katika wilaya ya kaskazini ya Ngorongoro waliishtumu serikali kwa kujaribu kuwalazimisha kuondoka kwenye ardhi ya mababu zao ili kuandaa mashindano ya uwindaji kwa watalii kutoka nje.
Lakini serikali ilitupilia mbali tuhuma hizo, ikidai kuwa inataka kulinda kilomita za mraba 1,500 za eneo hilo kutokana na shughuli za binadamu ili kusaidia wanyamapori kustawi.
Huku hali ya mvutano ikiongezeka, wakati mwingine maandamano yaligeuka kuwa vurugu, ambapo makabiliano yalizuka mwezi Juni huko Loliondo kati ya polisi na waandamanaji wa Kimasai.
Waandamanaji 25 wa Kimasai walishtakiwa kwa mauaji baada ya afisa wa polisi kufariki katika makabiliano hayo.
Mmasai mmoja aliachiliwa wakati huo lakini wengine walibaki gerezani tangu mwezi Juni.
Wakili wao Yonas Masiaya amesema waendesha mashtaka katika mahakama ya Arusha leo Jumanne wamefuta mashtaka yote.