Waathiriwa wa ukatili wa kundi la waasi la Lord's Resistance Army, LRA, nchini Uganda, wamekuwa na maoni mseto, kuhusu mipango ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuanzisha kesi dhidi ya kiongozi mtoro wa kundi hilo, Joseph Kony, bila kuwepo mahakamani.