Rais Paul Biya wa Cameroon anaadhimisha miaka 40 madarakani huku maswali mengi yakiulizwa kuhusu kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 89. Biya hajaonekana hadharani tangu Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kutembelea taifa hilo la Afrika ya Kati mwezi Julai.