Mazungumzo, yamepangwa kufanyika nchini Afrika Kusini, yatalenga katika kumaliza vita vya miaka miwili ambavyo vimeua malefu ya watu watu.
Tangazo kutoka kwa mshauri wa taifa wa usalama Redwan Hussein limekuja siku kadhaa baada ya serikali ya shirikisho kutangaza kukamata miji mitatu muhimu huko Tigray, pamoja na Shire, ambao ni mwenyeji wa idadi kubwa ya watu ambao wamebanduliwa na vita.
Katika siku za karibuni, wanadiplomasia wameisihi serikali ya shirikisho na majeshi ya Tigray kukubali sitisho la haraka la mapiano, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterress akionya Jumatatu kwamba hali kaskazini mwa Ethiopia “inatoka nje ya udhibiti.”
Mazungumzo ya amani ambayo yanaongozwa na Umoja wa Afrika yalipangwa awali kufanyika mapema mwezi huu nchini Afrika Kusini, huku wote waasi wa Tigray na serikali ya shirikisho wakisema walikuwa tayari kushiriki. Mazungumzo yalicheleweshwa kutokana na masuala ya kiufundi.
Redwan alisema kwenye Twitter Alhamisi kwamba serikali ya shirikisho “imethibitisha tena nia yetu ya dhati kushiriki” katika mazungumzo ambayo yanasimamiwa na AU.
“Hata hivyo, tumesikitishwa kwamba baadhi wamepania kuvura mazungumzo ya amani na kusambaza tuhuma za. Uongozi dhidi ya hatua za kujihani,” aliongezea, akizungumzia siyo moja kwa moja taarifa za karibuni kutoka kwa maafisa wa Magharibi wakielezea wasi wasi juu wa ripoti za mashambulizi kwa raia.
Serikali ya shirikisho ilisema wiki hii kwamba ilikuwa inapanga kuchukua udhibiti wa viwanja vya ndege huko Tigray na taasisi za serikali ya shirikisho ili “kulinda utaifa na eneo la nchi.”
Mkuu wa sera za mambo ya nje katika EU Josep Borrell alisema Jumatatu kwamba “EU imesikitishwa sana na kusambaa kwa ghasia na gharama isiyoweza kurekebishwa kwa maisha ya mwanadamu” nchini Ethiopia na kuzisihi pande zianze mazungumnzo ya amani “bila ya kuchelewa.”
Ripoti ya karibuni ya UN imegundua kwamba pande zote zimetenda ukiukaji wa haki za binadamu tangu mzozo ulipozuka Novemba mwaka 2020.
Samantha Power, ambaye anaongoza USAID alionya Jumapili kwamba kkuan “hatari kubwa na mashambulizi zaidi na mauaji ambayo yametendwa dhidi ya raia” kama mapigano yataingia katika kambi za wasiokuwa na makazi huko Tigray.
Waasi wa Tigray hakupatikana haraka kuthibitisha ushiriki wao katika mazungumzo ya Afrika Kusini ya Oktoba 23 lakini awali walielezea nia ya dhati ya kushiriki katika mazungumzo ya amani ambayo yanasimamiwa na AU.