Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:25

Kifungo cha miaka 5 jela Uganda ukisambaza habari kwenye whatsapp, facebook.


Rais wa Uganda Yoweri Museveni akisaini mojawapo ya miswada yeye utata na kuwa sheria.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni akisaini mojawapo ya miswada yeye utata na kuwa sheria.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesaini mswaada wa matumizi ya mitandao ya kijamii na kuwa sheria na hivyo kuwaweka watumiaji wa mitandao hiyo katika hatari ya kufungwa hadi miaka 5 gerezani endapo watachapisha au kusambaza haabri ambazo zinaikera serikali au watu binafsi.

Sheria hiyo yenye utata wanaharakati wa kutetea uhuru wa kujieleza na habari wanasema ni ya kukandamiza uhuru wa kujieleza.

Mojawapo ya vipengele kwenye sheria hiyo inahusu matumizi ya mitandao ya kijamii katika kikao cha bunge mwezi Septemba.

Museveni amesaini sheria hiyo aAhamisi wiki hii.

“Mtu yeyote anayetumia mitandao ya kijamii kuchapisha habari, kusambaza habari ambazo zimepigwa marufuku kulingana na sheria za Uganda, or kuficha jina lake au picha halisi, anavunja sheria,” inasema sheria hiyo mpya.

“Anayechapisha habari kwenye mitandao ya kijamii au kusambaza habari iliyochapishwa, anawajibika. Iwe ni mtu binafsi au shirika,” inaendelea kusema sheria hiyo.

Inaweka marufuku kwa mtu yeyote kupata taarifa za mtu mwingine bila idhini, kusambaza habari kuhusu watoto bila idhini ya mzazi, kutuma au kusambaza habari za uchochezi, na kutuma au kusambaza habari ambazo zinaweza kuharibu sifa ya mtu.

Wanaharakati wanataka sheria kufutwa

Bunge la Uganda, Kampala, Sept. 28, 2017.
Bunge la Uganda, Kampala, Sept. 28, 2017.

Mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu habari na mawasiliano Moses Magogo, amesema sheria hiyo ilitungwa kwa kuzingatia haja ya kuilinda kila mtu anayetumia na asiyetumia mitandao ya kijamii na kwamba maisha ya watu yamekuwa yakiingiliwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, wakosoaji wanataka sheria hiyo kufutwa, wakisema kwamba inakandamiza uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari.

Sheria hiyo ilipitishwa na bunge Septemba 8, 2022. Inatoa adhabu ya kifungo cha hadi miaka 5 gerezani au faini ya dola 2,619 (Shilingi milioni 10 za Uganda) au kufungwa jela na pia kulipa faini.

Sheria hiyo inalenga watumiaji wa mitandao yote ya kijamii kama YouTube, WhatsApp, Facebook, Instagram, Twitter, WeChat, TikTok, Sina Weibo, QQ, Telegram, Snapchat, Kuaishou, Qzone, Reddit, Quora, Skype, Microsoft Team na Linkedin.

Tozo kwenye mitandao ya kijamii

Nembo ya mtandao wa kijamii wa facebook
Nembo ya mtandao wa kijamii wa facebook

Mnamo mwaka 2018, serikali ya Uganda ilianzisha tozo ya kila siku kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Baada ya hatua hiyo kufeli, serikali ilianzisha tozo ya asilimia 12 kwa mtu yeyote anayenunua kifurushi cha internet.

Serikali ya Uganda imekuwa ikifunga mitandao ya kijamii na huduma ya internet kila mara hasa wakati wa uchaguzi.

Mtandao wa kijamii wa facebook ulifungwa Januari 2021 ulifungwa kutokana na amri ya serikali, lakini raia wa Uganda wamekuwa wakitumia mfumo wa siri wa kupata Facebook, maarufu VPN.

XS
SM
MD
LG