Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 14, 2025 Local time: 04:53

Vladmir Putin na rais Xi Jinping watakutana wiki ijayo huko Uzbekistan


Rais wa Russia Vladimir Putin alipokutana na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan mjini Vladivostok.Valery Sharifulin/TASS .
Rais wa Russia Vladimir Putin alipokutana na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan mjini Vladivostok.Valery Sharifulin/TASS .

Rais wa Russia Vladmir Putin na rais wa China Xi Jinping watakutana wiki ijayo katika mkutano huko Uzbekistan, afisa mmoja wa Russia amesema jumatano.

Viongozi hao wawili watakutana katika mkutano wa shirika la ushirikiano la Shanghai, unaofanyika katika mji wa Samarkand nchini Uzbekistan hapo Septemba 16 na balozi wa Russia nchini China, Andrei Denisov, aliwaambia waandishi wa habari. Chini ya siku kumi kutoka sasa mkutano mwingine wa viongozi wetu utafanyika katika mkutano wa SCO huko Samarkand.

Tunajiandaa kikamilifu kwa hilo, Denisov alinukuliwa na shirika la habari la serikali ya Russia, Tass. Ziara ya Uzbekistan ikiwa itaendelea, itakuwa ziara ya kwanza ya kigeni ya Xi katika miaka miwili na nusu.

Vyombo vya habari vya Russia pia vimeripoti mipango ya Xi kuitembelea Kazakhstan kabla ya mkutano wa kilele nchini Uzbekistan, lakini ripoti hizo bado hazijathibitishwa. Alipoulizwa kuhusu ziara ya Uzbekistan, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China, mao Ning aliuambia mkutano wa kila siku Jumatano, kwamba kwa swali lako sina cha kuelezea.

XS
SM
MD
LG