Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 03:07

Guangzhou imeweka vizuizi vya COVID-19 katika sehemu za jiji hilo

Vipimo vya Corona China.
Vipimo vya Corona China.

Guangzhou China siku ya Jumatano iliweka vizuizi vya COVID-19 katika sehemu za jiji hilo ikiungana na Shenzhen katika kupambana na milipuko ya ndani, ikizidisha kutokuwa na uhakika juu ya biashara na maisha ya kila siku katika miji miwili ya kusini mwa China yenye nguvu zaidi kiuchumi.

Miji mikubwa kadhaa ya China imeongeza vizuizi vyao vya COVID-19 wiki hii, na kuathiri shughuli za mamilioni ya watu. Kwa kuzingatia kusawazisha mahitaji ya kiuchumi na juhudi za kudhibiti kila milipuko, viongozi walisema vizuizi vitadumu kwa siku chache tu, ingawa miji mingine midogo iliongeza vizuizi mapema mwezi huu.

Sera ya China inayoitwa "dynamic Covid zero" inaifanya kuwa ya tofauti wakati nchi zingine polepole zinaibuka kutoka kwenye vizuizi vya corona licha ya gharama kwa uchumi wa pili kwa ukubwa ulimwenguni ambao tayari unakabiliwa na ukuaji wa polepole.

XS
SM
MD
LG