Makombora ya Russia yalifyatuliwa katika miji ya Ukraine iliyo karibu na kiwanda cha nyuklia cha Zapori-zhzhia usiku kucha. Maafisa wa eneo hilo walisema siku ya Jumapili, na kuongeza wasiwasi kwa wakaazi huku ripoti kuzunguka mtambo huo zikizidisha hofu ya maafa ya kuvuja kwa mionzi.