Siku moja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kutangaza kuna ugonjwa usiojulikana katika mkoa wa Lindi nchini humo naye Mganga mkuu wa Serikali Dr. Aifello Sichwale amethibitisha hadi kufikia Julai 12 kulikuwa na wagonjwa 13 kati yao watatu wamefariki kutokana na ugonjwa huo usiojulikana