Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 08:04

R Kelly ahukumiwa miaka 30 jela


Picha ya kuchorwa inamuonyesha wakili Jennifer Bonjean akimpa pole R Kelly wakati alipohukumiwa mjini New York
Picha ya kuchorwa inamuonyesha wakili Jennifer Bonjean akimpa pole R Kelly wakati alipohukumiwa mjini New York

Robert Kelly, mwanamuziki Mmarekani maarufu kama R Kelly, Jumatano alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kutumia umaarufu wa nyimbo zake za R&B kuwanyanyasa kingono wasichana ambao walikuwa mashabiki wake.

Mwimbaji huyo na mtungaji wa nyimbo alipatikana na hatia ya ulaghai na biashara haramu ya ngono mwaka jana katika kesi ambayo iliwapa moyo waliomshtaki ambao waliwahi kujiuliza ikiwa hadithi zao zilipuuzwa kwa sababu walikuwa wanawake weusi.

Jaji wa wilaya ya New York Ann Donnely alitoa hukumu hiyo mahakamani katika mji wa Brooklyn. Hukumu hiyo ni pigo kwa Kelly, mwenye umri wa miaka 55. Aliendelea kupendwa na mashabiki wengi hata baada ya madai kuhusu kuwanyanyasa wasichana wadogo kuanza kusambaa hadharani mwaka wa 1990.

Wakitokwa na machozi na wakionekana wenye hasira, waliomshtaki R Kelly waliiambia mahakama Jumatano kwamba aliwadhulumu na kuwapotosha mashabiki wake, wakati nyota huyo wa zamani wa R&B akisubiri kuhukumiwa kwa kosa la biashara haramu ya ngono.

“Ulinifanya nifanye mambo ambayo yalinivunja moyo. Nilitamani kufa kwa sababu ya jinsi ulivyonifanya nijihisi duni,” mwanamke mmoja alimwambia mwimbaji huyo aliyewahi kushinda tuzo ya juu ya Grammy.

Alisema alipatwa na kiwewe tangu wakati huo kufuatia hali alioipitia wakati wa ujana wake.

Mwanamke wa tatu, akilia na kuvuta pumzi wakati akiongea, alisema kuhukumiwa kwa Kelly kumerejesha imani yake katika mfumo wa sheria. Alisema Kelly alimdhulumu baada ya kuhudhuria tamasha yake akiwa na umri wa miaka 17.

XS
SM
MD
LG