Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 04:36

Marais wanakutana kujadili usalama DRC


Wanajeshi wa DRC katika mapambano dhidi ya waasi wa M23. PICHA: Reuters
Wanajeshi wa DRC katika mapambano dhidi ya waasi wa M23. PICHA: Reuters

Viongozi wa jumuiya ya Afrika mashariki wanakutana Nairobi kenya na kujadiliana kuhusu vita vinavyoendelea mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Hii ni baada ya kundi la waasi la M23 kudhibithi mji wa Bunagana. Sehemu hiyo pia imeshuhudia ongezeko la ujumbe wa chuki katika jamii. Mkutano wa viongozi hao ni wa tatu kujadili hali ya usalama DRC.

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo haitaki wanajeshi wa Rwanda kushirikishwa katika jeshi la pamoja kwa ajili ya kupambana na waasi mashariki mwa DRC.

DRC imesema kwamba inakubali pendekezo la rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kutuma jeshi la jumuiya ya Afrika mashariki nchini humo, kupambana na waasi wa M23, lakini haiwezi kuruhusu wanajeshi wa Rwanda kuwa sehemu ya mpango huo.

Mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika mashariki Uhuru Kenyatta, alitangaza wiki iliyopita kwamba jeshi la jumuiya hiyo linastahili kuingia DRC mara moja na kupambana na makundi ya waasi mashariki mwa nchi hiyo. Kenyatta alisema uwamuzi huo ulifikiwa baada ya kushauriana na marais wenzake wa jumuiya ya Afrika mashariki.

Taarifa ya ikulu ya Nairobi ilisema kwamba jeshi hilo litashika doria katika sehemu za Ituri, North Kivu na South Kivu na kusaidia jeshi la DRC kwa ushirikiano na jeshi la umoja wa mataifa MONUSCO.

Kenyatta alitaka sehemu za Ituri, Noth Kivu ikiwemo Bunagana, Bugusa, sehemu za Petit Nor, Masisi, Lubero, Beni-kasindi, na sehemuza South Kivu kutangazwa kuwa sehemu ambazo silaha haziruhusiwi bila idhini ya serikali na kwamba makundi yote yanayobeba silaha yapokonywe silaha hizo kwa lazima.

Makamanda wa jeshi kutoka majeshi ya nchi zinazoshiriki, walikutana Nairobi Jumapili tarehe 19 kuweka mikakati ya kuingia DRC.

XS
SM
MD
LG