Ofisi ya mambo ya nje ya Uingereza imesema kwamba kati ya waliowekewa vikwazo hivyo ni Alexander Ananchenko na Sergey Kozlov, ambao imewataja kuwa watu waliojitangaza kuwa waziri mkuu na mwenyekiti wa serikali zinazojiita Donetsk na jamhuri ya watu wa Luhansk.
Wengine waliowekewa vikwazo ni watu kutoka familia ya maafisa wa ngazi ya juu katika serikali ya Russia, wakiwemo Pavel Ezubov, ambaye ni ndugu wa bilionea wa Russia Oleg Deripaska, na Nigina Zairova, ambaye ni msaidizi mkuu wa mfanyabiashara Mikhail Fridman.
Mke wa waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergey Lavrov, Maria Lavrova, amewekewa vikwazo vya kutosafiri, pamoja na mali zake.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Liz Truss amesema kwamba wataendelea kuwawekea vikwazo watuw anaofanikisha vita vya Russia dhidi ya Ukraine.
Serikali ya Uingereza vile vile imetangaza kwamba itapiga marufuku uagizaji wa bidhaa za chuma kutoka Russia.