Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 10:49

Nigeria: Jaji apiga marufuku ufuatiliaji wa habari kuhusu ugaidi


Uharibifu uliotekelezwa na kundo la wapiganaji wa Boko Haram mjini Maiduguri, Nigeria, April 27, 2018. PICHA: REUTERS
Uharibifu uliotekelezwa na kundo la wapiganaji wa Boko Haram mjini Maiduguri, Nigeria, April 27, 2018. PICHA: REUTERS

Jaji wa mahakama ya serikali kuu ya Nigeria ameamuru kwamba kesi zote za ugaidi nchini humo hazitafanyika mbele ya kamera.

Jaji John Terhemba Tsoho, vile vile amesema kwamba hakuna waandishi hawataruhusiwa kufuatilia kesi hizo mahakamani.

Amesema kwamba amri hiyo mpya inalenga kuhakikisha usalama wa wahusika wote katika kesi za Ugaidi, raia na kuhakikisha kwamba haki inapatikana.

Kwingineko, kiongozi wa kundi lililopigwa marufuku la watu wa Biafra IPOB, Nnamdi Kanu, ambaye alifunguliwa mashtaka ya ugaidi, amewasilisha mashtaka mahakamani akidai kwamba hawezi kushitakiwa kwa sababu alisafirishwa kutoka Kenya kinyume cha sheria.

Nnamdi Kanu, alikimbia kutoka Nigeria baada ya kukosa kufika mahakamani mwaka 2017, alipokuwa ameachiliwa kwa dhamana.

XS
SM
MD
LG