Mchumba wa mwandishi aliyeuawa wa gezeti la Washington Post la Marekani, Jamal Khashoggi aliapa Alhamis kuendelea kupigania haki.
Maoni yake yalikuja wakati mahakama ya Uturuki ilipotoa uamuzi wa kusitisha kesi ya raia 26 wa Saudi Arabia, walioshtakiwa kwa mauaji na kuihamishia kesi hiyo Saudi Arabia. Khashoggi, mwandishi wa gazeti la Washington Post aliuawa wakati alipoutembelea ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Instanbul hapo Oktoba mwaka 2018 kwa ajili ya kukusanya nyaraka zinazohitajika kumuoa Hatice Cengiz.
Akizungumza na wanahabari baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo Alhamis, Cengiz alisema atakata rufaa dhidi ya kesi hiyo. Hatutakata tamaa kwa sababu tu, mchakato wa mahakama umechukua uamuzi kama huu hivi sasa Cengiz alisema.
Nitaendelea na mchakato wa kisheria kadri niwezavyo. Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mwaka 2020 baada ya Saudi Arabia kukataa ombi la Uturuki la kuwarejesha washtakiwa.