Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 18:07

Jumuia ya kimataifa yalani mapinduzi ya kijeshi Burkina Faso, raia washerekea kuondolewa kwa serikali


Raia washikilia bendera ya taifa ya Burkina Faso, wakikusanyika mjini Ouagadougou kuunga mkono mapinduzi ya kijeshi, Januari 22, 2022. Picha ya AFP
Raia washikilia bendera ya taifa ya Burkina Faso, wakikusanyika mjini Ouagadougou kuunga mkono mapinduzi ya kijeshi, Januari 22, 2022. Picha ya AFP

Jumuia ya uchumi ya nchi za Afrika magharibi (ECOWAS) imelani mapinduzi ya kijeshi  yaliyofanyika nchini Burkina Faso jana Jumatatu na kuwataka wanajeshi kurudi kambini, na imeomba kufanyike majadiliano na viongozi wa kiraia kutafuta suluhu nchini humo.

Naye Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guteress amewataka viongozi wa kijeshi kumuachilia huru mara moja rais Roch Marc kabore anaeshikiliwa na wanajeshi pamoja na mawaziri wake.

Wakati huo huo zaidi ya watu 1,000 walikusanyika katika mji mkuu Ouagadougou ili kuonyesha uungaji mkono wao kwa mapinduzi ya kijeshi.

Baraza jipya la utawala lililopewa jina la MPSR linaongozwa na Luteni Kanali Paul Henri Sandaogo Dambia lilifunga mipaka ya nchi, kuweka amri ya kutotoka nje usiku, kusitisha katiba na kuvunja serikali na bunge, na kusema kwamba litairejesha nchi kwenye uongozi wa kikatiba, bila pamoja na hivo kusema lini litafanya hivo.

XS
SM
MD
LG