Leakey amefariki akiwa na umri wa miaka 77.
Kazi yake ilipelekea kutambuliwa kwa bara la Afrika kuwa mahali ambapo uhai wa binadamu ulianzia.
Aliongoza kampeni ya kupinga uwindaji haramu nchini Kenya, na kupelekea kuchomwa moto kwa pembe za ndovu zilizokuwa zimepatikana kutokana na uwindaji haramu.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kwamba Leakey aliitumikia Kenya kwa hali ya kipekee.
Leakey alihudumu katika serikali ya Kenya katika nyadhifa mbali mbali ikiwemo katika makumbusho ya kitaifa ya Kenya, shirika la kitaifa la kuwahudumia Wanyama pori KWS na kuwa mkuu wa huduma kwa umma.
Akiwa na umri wa miaka 20, alifanya ugunduzi muhimu kuhusu walipotokea watu wa bahari na ukoo wa kale wa watu wa sasa.
Kazi yale ilipelekea kuwepo kwa ushahidi kwamba binadamu wa kwanza waliishi barani Afrika.
Aliongoza shirika la kuhifadhi Wanyama pori nchini Kenya, miaka ya 1980 wakati uwindaji haramu ulikuwa umewekwa hatarini maisha ya ndovu na vifaru.
Wakati huo, alitoa maagizo kwa maafisa wa kulinda Wanyama pori, kuwapiga risasi na kuwaua wawindaji haramu papo hapo.