Uingereza imeripoti ongezeko kubwa la maambukizi ya aina mpya ya virusi vya Corona, Omicron.
Kati ya watu 119,000 na 106,000 wanaripotiwa kuambukizwa Omicron kila siku nchini Uingereza.
Idadi kubwa ya aviwanda na mashirika ya usafiri yanakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi kutokana na wafanyakazi kutakiwa kujitenga baada ya kugunduliwa kuambukizwa virusi hivyo.
Maambukizi ya virusi vya Omicron yamekuwa yakiongezeka kwa kasi sana nchini Uingereza katika mda wa siku saba zilizopita.
Watu 679,165 wamegunduliwa kuambukizwa katika muda wa wiki moja.
Serikali imepunguza mda wa wagonjwa kujitenga kutoka siku 10 hadi saba ili kuhakikisha kwamba wanarejea kazini.
Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema kwamba huenda serikali ikachukua hatua kali kukabiliana na maambukizi iwapo yataendelea kuongezeka.