Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 29, 2024 Local time: 11:45

Vyombo vya habari vyafungwa Afghanistan


Vyombo vya habari nchini Afghanistan vinakumbana na mazingira magumu ya kufanya kazi kutokana na uhaba wa pesa tangu wapiganaji wa Taliban walipochukua uongozi wa taifa hilo.

Ripoti ya waandishi wa habari wasiokuwa na mipaka, iliyoandikwa kwa ushirikiano na chama cha waandishi huru wa habari wa Afghanistan, inaonyesha kwamba asilimia 43 ya vyombo vya habari nchini humo vimefungwa na kupelekea asilimia 60 ya waandishi kupoteza ajira.

Ripoti hiyo vile vile inasema kwamba utawala wa Taliban umebadilisha kabisa namna habari zinavyoandikwa nchini humo.

Vituo vya Habari 312 pekee ndiyo vinaendelea kufanya kazi nchini humo, kati ya 543 vilivyosajiliwa. 231 vimefunga na karibu waandishi wa habari 6,400 kupoteza ajira.

Mojawapo ya sababu kuu ya vituo hivyo kufunga shughuli zao ni mazingira magumu ya kufanya kazi yaliyowekwa na utawala wa Taliban.

XS
SM
MD
LG