Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 00:04

Hatma ya tukio la mkesha wa mwaka mpya Times Square, New York kujulikana siku ya Krismas


Meya wa jiji la New York, Bill de Blasio, Jumapili amesema uamuzi utatolewa siku ya Krismas kuhusu kufanyika ama la tukio la sherehe za mwaka mpya kama inavyofanyika katika miaka ya nyuma kabla ya kuzuka janga la Covid-19.

Kutokana na hivi sasa kuwepo kwa aina mpya ya virusi vya Omicron ambavyo vinasambaa katika jiji hilo, maafisa wanajipanga kufanikisha upimwaji watu huku kukiwa na mahitaji makubwa zaidi.

Mwaka jana sherehe za mkesha wa mwaka mpya katika eneo la Times Square zilifanyika kwa njia ya kuzungatia watu kujitenga, na kuhudhuriwa na kundi dogo la watu ambao walikuwa ni wafanyakazi wa makundi muhimu.

Meya de Blasio mwezi Novemba alitangaza kwamba tukio hilo mashuhuri la mwaka mpya litafanyika kama kawaida na watakao hudhuria watatakiwa waonyeshe kama wamechanjwa, na wale ambao hawajachanjwa kwa sababu mbalimbali itawabidi waonyeshe uthibitisho wa kutokuwa na maambukizi ya Covid-19.

XS
SM
MD
LG