Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 08:45

Kiongozi wa upinzani katika uchaguzi wa Sierra Leone kufunguliwa mashtaka ya ufisadi


Samura Kamara kiongozi wa upinzani nchini Sierra Leone akiwa katika kampeni mwaka 2018.
Samura Kamara kiongozi wa upinzani nchini Sierra Leone akiwa katika kampeni mwaka 2018.

Tume ya kupambana na ufisadi ya Sierra Leone imewapata na makosa ya ulaji rushwa maafisa sita akiwemo mwanasiasa wa upinzani maarufu anayetarajiwa kugombea urais kwa tiketi ya vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2023.

Samura Kamara alikuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha upinzani cha All People's Congress (APC) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2018.

Vyama vya upinzani vimepanga kumteua kugombea urais katika uchaguzi ujao.

Wengine na maafisa wa ngazi ya juu serikali akiwemo mhasibu wa sasa katika ubalozi wa Sierra Leone katika Umoja wa Mataifa, New York, Marekani.

Wastuhumiwa hao sita wanakabiliwa na mashtaka kadhaa ya ufisadi kuhusiana na wizi wa dola milioni 4.2 zilizokuwa zimepangiwa kutumiwa kwa ukarabati wa ubalozi mdogo wa Sierra Leone, Manhattan.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na tume ya kupambana na ufisadi, Kamara anakabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo matumizi mabaya ya pesa za uma, kiasi cha dola 2,560,000 zilizokuwa zimepangiwa kwa ukarabati wa ubalozi huo mdogo.

Alikuwa Waziri wa mambo ya nje wakati ufisadi unaodaiwa ulipofanyika.

Kamara amesema kwamba timu yake ya mawakili inasoma mashtaka ya tume hiyo.

Timu yake ya kampeni imesema kwamba hakufanya kosa lolote ikieleza kwamba “miaka yake 40 katika huduma ya uma, ilikuwa ya uadilifu na hajawahi kuhusishwa ndani na nje ya nchi kuhusiana na kashfa yoyote”.

Mamia ya wafuasi wa upinzani walimsindikiza wakati alipofikishwa mbele ya tume ya kupambana na ufisadi, kuhojiwa katika mji wa Freetown, mapema mwezi huu.

Amesema kwamba mashtaka dhidi yake yamechochewa kisiasa.

Wafuasi wake wamekabiliana na maafisa wa polisi, waliotumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya.

Kamara na wenzake wanatarajiwa kufikishwa mahakamani Desemba tarehe 10.

XS
SM
MD
LG