Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 04:57

Maandamano yaendelea Sudan


Maelfu ya raia wa Sudan wameandamana katika mitaa ya Khartoum, na miji mingine Alhamisi, kuendelea kutoa msukumo kwa viongozi wa kijeshi.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuingia katika makubaliano ambayo yamemrejesha waziri mkuu raia baada ya mapinduzi mwezi uliopita.

Vyama maarufu vya siasa na vuguvugu lenye nguvu la maandamano kwa pamoja wamepinga uamuzi wa Jumapili wa waziri mkuu Abdalla Hamdok kusaini makubaliano na jeshi.

Hatua ya waziri mkuu inaonekana kama usaliti ama wakisema inatoa kinga ya kisiasa kwa mapinduzi.

Waandamanaji katika mji wa Al Daim waliimba kwamba mapinduzi yanatoka kwa watu na wanajeshi warudi kambini.

Vilevile wanataka kutendewa haki wale wote waliopoteza maisha katika maandamano ya awali.

Waandamanaji pia walifunga barabara kuu kwenye kitongoji cha Sahafa katika mji mkuu, wakiwa na bendera za Sudan na kuimba Burhan huto tawala, uondolewe utawala wa kijeshi.

XS
SM
MD
LG