Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:54

Waziri wa zamani wa Msumbiji kuletwa Marekani kukabiliana na mashitaka ya rushwa


Waziri wa zamani wa fedha wa Msumbiji, Manuel Chang, ambaye kwa sasa ameshikiliwa nchini Afrika Kusini, atasafirishwa kuja Marekani kukabiliana na mashitaka ya kashfa ya dola bilioni mbili mahakama imeamua.

Chang alikuwa anashikiliwa Afrika Kusini toka mwaka 2018 kwa maombi ya serekali ya Marekani, juu ya kushutumiwa kuhusika katika deni kubwa lililokuwa limefichwa.

Kashfa hiyo ambayo ilifichuka kuhusiana na mkopo ambao ulitoweka ukiwa na lengo la kuboresha taifa la Msumbiji, uligeuka na kuwa msukosuko mkubwa wa kifedha na kusababisha maelfu ya watu kuingia katika umasikini.

Jaji wa mahakama kuu ya Afrika Kusini, Margaret Victor, amesema bwana Manuel Chang atakabidhiwa na kusafirishwa kwenda Marekani kukabiliana na mashitaka yanayo mkabili.

XS
SM
MD
LG