Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 19:21

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani yasema muda ni mdogo kushughulikia mgogoro wa Ethiopia


Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Jumatatu imesema Washington ina-amini kutakuwa na kipindi cha muda mfupi cha kufanyakazi na Umoja wa Afrika kuendelea kutatua mgogoro wa Ethiopia kwa amani wakati mwakilishi maalumu wa Marekani atakapo rejea Addis Ababa.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Ned Price, amesema Jeffrey Feltman, mwakilishi maalumu wa Marekani kwa pembe ya Afrika, atakutana na mwakilishi wa Umoja wa Afrika katika eneo hilo rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, siku ya Jumatatu usiku.

Washington imeweka wazi ikitaka kumalizika kwa mapigano yaliyodumu kwa mwaka mzima sasa juu ya mgogoro wa eneo la kaskazini mwa Ethiopia baina ya serekali na vikosi vya Tigray, mapigano ambayo yameongezeka zaidi katika wiki za karibuni.

Vikosi vya Tigray na washirika wake wametishia kusonga mbele mpaka Addis Ababa.

XS
SM
MD
LG