Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 14:37

ETHIOPIA: Waziri mkuu ahimiza raia kupigana na kundi la TPLF


Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Makundi mawili tofauti yanayopigana na serikali kuu ya Ethiopia yamesema kwamba yamedhibithi miji kadhaa, wakati Waziri mkuu wa nchi hiyo akiwahimiza raia kuchukua silaha na kupigana na makundi hayo.

Mapigano hayo yanatishia kuyumbisha zaidi hali ya utulivu ya Ethiopia ambayo ni ya pili Afrika kwa idadi kubwa ya watu.

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, amewahimiza raia kupigana dhidi yaTigray People’s Liberation Front TPLF, chama kinachodhibithi mkoa wa kaskazini wa Tigray.

Abiy ametoa wito huo baada ya wapiganaji wa Tigray kusem akwamba wamethibithi mji mwingine kwenye barabara kuu inayounganisha sehemu za kaskazini na mji mkuu wa Addis Ababa na nchi Jirani ya Djibouti.

Abiy ameandika ujumbe wa facebook kwamba raia wa Ethiopia wanastahili kutumia kila aina ya silaha walio nayo kupigana na kuwashinda magaidi wa TPLF. Msemaji wa TPLF Getachew Reda, amesema kwamba wapiganaji hao wamedhibithi mji wa Kombolcha na uwanja wake wa ndege katika eneo la Amhara.

XS
SM
MD
LG