Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:45

Wauguzi wa Kenya wafeli kiingereza kufanya kazi Uingereza


Wauguzi wa Kenya katika maandamano kudai malipo bora Dec. 8, 2016.
Wauguzi wa Kenya katika maandamano kudai malipo bora Dec. 8, 2016.

Wafanyakazi kadhaa wa afya nchini Kenya wamefeli mtihani wa kiingereza ambao ungewawezesha kupata nafasi za kazi nchini Uingereza.

Waziri wa afya wa Kenya Mutahi Kagwe, amesema kwamba wafanyakazi wa afya 10 pekee ndio walipita mtihani huo wa kiingereza, kati ya wafanyakazi 300 walioomba kazi nchini Uingereza.

Kiingereza na Kiswahili ndizo lugha rasmi zinazotumika katika vyuo vikuu na kote nchini Kenya.

Kenya ilisaini makubaliano na Uingereza mwezi July, kuwaruhusu wafanyakazi wa afya wa Kenya kufanya kazi Uingereza. Mpango huo unatoa fursa kwa wafanakazi wa afya ambao wamesomea kazi hiyo lakini hawana ajira.

Kufiakia sasa, wafanyazi wa afya 900 kutoka Kenya, wameajiriwa Uingereza.

XS
SM
MD
LG