Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 16:39

ANC chakabiiliwa na ushindani mkali katika uchaguzi wa manispaa


Wafuasi wa chama cha ANC katika kampeni
Wafuasi wa chama cha ANC katika kampeni

Chama kinachotawala nchini Afrika kusini cha African national congress ANC, kinakabiliwa na ushindani mkubwa katika uchaguzi wa manispaa, kutokana na rekodi mbovu ya maendeleo katika sehemu ambazo kwa miaka mingi, kimekuwa na ufuasi mkubwa.

Chama cha ANC, kina matumaini ya kushinda kura nyingi katika miji mikubwa kilipoteza kwa upinzani katika uchaguzi wa mwaka 2016, ambapo kilipoteza viti vingi zaidi tangu kilipoingia madarakani kikiongozwa na Nelson Mandela, mwaka 1994.

Wachambuzi wa siasa wanatabiri kwamba chama cha ANC kitaendelea kufanya vibaya katika uchaguzi huo wakisema ufuasi wake huenda ukashuka chini ya asilimia 50.

Barabara zimeharibika, kuna ukosefu wa maji na nguvu za umeme katika sehemu kadhaa kama steel belt, Gauteng na sehemu za Johannesburg zilizokuwa ngome ya chama cha ANC.

Kiongozi wa ANC Cyril Ramaphosa, akiwa katika kampeni, amesema kwamba chama hicho kimejifunza kutokana na makosa yake na kitahakikisha kwamba sehemu za manispaa zinasimamiwa vyema.

Kuna madai ya kuwepo ufisadi, ubaguzi na ukosefu wa ajira katika usimamizi wa manispaa.

XS
SM
MD
LG