Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 20:35

DRC: Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi aapisha. kanisa, wapinzani wapinga uteuzi wake


mkuu mpya wa tume ya uchaguzi DRC Denis Kadima
mkuu mpya wa tume ya uchaguzi DRC Denis Kadima

Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ameapishwa licha ya kuwepo pingamizi kuhusu uteuzi wake.

Denis Kadima anachukua nafasi hiyo ya tume huru ya kitaifa ya kusimamia uchaguzi CENI, wakati kuna mzigo mkubwa wa kuandaa uchaguzi mkuu mwaka 2023.

Uteuzi wake umepingwa na makundi kadhaa yakiwemo ya kidini yakitaka uteuzi kufanyika baada ya mazungumzo na makubaliano ya wahusika wakuu katika uchaguzi.

Kanisa katoliki na la waprotestanti wamepinga uteuzi wake kwa msingi kwamba haukufuata kanuni.

Madai yao yanaungwa mkono na wanasiasa wa upinzani ambao hawakuidhinisha uteuzi huo bungeni.

Bunge la jamhuri ya kidemokrasia ya Congo liliidhinisha uteuzi wa Kadima mnamo Oktoba 16 licha ya kukosekana makubaliano na makundi ya kidini.

Wiki iliyopita, rais Felix Tshisekedi aliidhinisha uteuzi wa Kadima na wanachama wengine wa tume hiyo.

Wanachama watatu wanaostahili kuwakilisha vyama vya upinzani hawajateuliwa lakini rais Tshisekedi ana matumaini kwamba wataungana na tume hiyo hivi karibuni.

XS
SM
MD
LG