Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 12:08

DRC Mojawapo ya nchi fisadi zaidi duniani


Rais wa DRC Félix Tshisekedi
Rais wa DRC Félix Tshisekedi

Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imetajwa kuwa miongoni mwa nchi fisadi zaidi duniani, ikiorodeshwa kua nchi ya 170 kati ya 180.

Hayo ni kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la transparency international, mwaka 2020.

Lakini mkaguzi mkuu wa fedha Jules Alingete, akizungumza na shirika la habari la AFP, amesema kwamba hali inaendelea kubadilika nchini humo.

Alingete amesema kwamba mamilioni ya Dola yamepatikana kati yam waka jana na mwaka huu katika juhudi za kukabiliana na ufisadi zinazoendeshwa na serikali.

“Ilikuwa lazima tukabiliane na watu waliokuwa wanaishi kama waliozaliwa ndani ya ufisadi. Watu wanaochukuliwa ufisadi na unyakuzi wa mali ya uma kama jambo la kawaida” amesema Alingete, akiongezea kwamba “uovu huo ulikuwa umekita mizizi na ilibidi tuchukue msimamo mkali sana. mbinu zetu zimeanza kuzaa matunda”.

Rais Felix Tshisekedi, ambaye aliingia madarakani mwaka 2019 kwa ahadi ya kupambana na ufisadi, aliteua Alingete mwenye umri wa miaka 58, kusimamia ofisi ya mkaguzi mkuu wa fedha, mwezi July mwaka uliopita.

Mapato ya serikali mnamo mwaka 2020, yalikuwa chini ya dola milioni 400 kila mwezi lakini Alingete anasema hivi sasa yameongeZeka na kufika hadi milioni 900.

Maafisa kadhaa katika serikali ya Congo, akiwemo gavana Atou Matubuana, wamefunguliwa mashtaka ya ufisadi katika siku za hivi karibuni.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG