Hata hivyo, kuna wasiwasi ya kutokea mapigano baada ya maelfu ya watu kushindwa kupiga kura kutokana na hali mbaya ya uslama, waasi wakiwa wanadhibithi sehemu kubwa ya nchi hiyo inayoorodheshwa kati ya nchi zenye misukosuko mingi sana duniani.
Tume ya uchaguzi imesema kwamba matokeo hayo yana maana kwamba hakuna duru ya pili ya uchaguzi itafanyika.
Aliyekuwa waziri mkuu Anicet George Pologuele, amemaliza katika nafasi ya pili akiwa na asilimia 21 ya kura huku Martin Ziguele akimaliza katika nafasi ya tatu na asilimia 7.
Kulikuwa na wagombea 16 wa urais wakiwemo wanawake watatu, katika uchaguzi mkuu wa urais Jamhuri ya Afrika ya kati.
Wagombea wa upinzani wamesema kwamba kulikuwepo udanganyifu mkubwa katika hesabu ya kura.
Uchaguzi huo ulifanyika licha ya mashambulizi ya muungano wa makundi ya waasi, ambayo yalisababisha maelfu ya watu kukosa kupiga kura.
Serikali imemshutumu aliyekuwa rais wa nchi hiyo François Bozizé, kwa kujaribu kufanya mapinduzi.
Bozize alizuiliwa kugombea urais.
Amekanusha madai kwamba anawaunga waasi kupindua serikali.
Waendesha mashtaka wameanzisha uchunguzi dhidi ya Bozize kuhusiana na madai ya kutaka kupindua serikali.
Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC