Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:46

Mauaji ya waandishi wa habari yanaendelea kuongezeka huku wakilengwa sana na wanasiasa, makundi ya uhalifu


Picha ya aliyekuwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi, aliyeuawa.
Picha ya aliyekuwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi, aliyeuawa.

Ripoti ya waandishi wa habari wasio na mipaka imesema kwamba zaidi ya waandishi wa habari 50 na wafanyakazi wengine katika sekta ya habari wameuawa mwaka huu 2020 wakiwa kazini, wengi wao wakiwa katika nchi ambazo hazina vita.

Idadi hiyo inaonyesha ingezeko la waandishi wa habari wanaouawa, wengi wao wakiwa waandishi wanaoandika habari za uchunguzi kuhusu uhalifu, ufisadi na maswala ya mazingira.

Mauaji mengi yametokea Mexico, India na Pakistan.

Ripoti ya waandishi wa habari wasio na mipaka inasema kwamba asilimia 84 ya waandishi wa habari ambao wameuawa mwaka huu walilengwa maksudi.

Mauaji mengi yametokea Mexico ambako waandishi nane waliuawa kutokana na kuandika habari kuhusu ulanguzi wa dawa za kulevya na kisiasa.

Hakuna mtu yeyote amefunguliwa mashtaka kuhusiana na mauaji ya waandishi wa habari nchini Mexico.

Mauaji mengine yamefanyika Afghanistan na Iran.

Pauline Adès-Mevel, ni mhariri mkuu na msemaji wa waandishi wa habari wasiokuwa na mipaka.

"Hata kama janga limepelekea baadhi ya ripoti kutoandikwa, waandishi wameendelea kushambuliwa. Waandishi wa habari wamejeruhiwa, wamelengwa wakati wa maandamano kote duniani. Tumeshuhudia hilo hivi karibuni nchini Ufaransa wakati wa sheria ya usalama wa dunia na katika maandamano ya kupinga sheria hiyo. Kwa hivyo, ni jambo tunaloliona kila mahali, tunayashuhudia katika umoja wa ulaya, Asia, Africa na Marekani hasa wakati wa maandamano ya George Floyd. Waandishi wanaoandika kuhusu maandamanao wanashambuliwa na wanalengwa sana.”

XS
SM
MD
LG