Wanasiasa wa upinzani nchini Ivory wamekataa kuvunja serikali yao ya mpito, waliounda baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika jumamosi, na ambao rais Alllasane Outtara alishinda mhula wa tatu madarakani.
Wanasiasa hao waliunda serikali yao baada ya kususia uchaguzi huo, wakidai kwamba hatua ya Ouattara kugombea mhula wa tatu madarakani ni kinyume cha katiba.
Baadhi ya wanasiasa hao wanazuiliwa na polisi majumbani mwao.
Na katika nchi jirani ya Guinea, mgogoro wa kisiasa unaendelea baada ya uchaguzi mkuu baada ya rais Alpha Conde kugombea urais kwa mhula wa tatu, hatua ambayo upinzani wanasema ni kinyume na katiba ya nchi hiyo.
Waekezaji katika nchi hizo mbili wameeleza wasiwasi kwamba migogoro hiyo huenda ikaathiri uchumi wa nchi hizo na kuhatarisha usalama katika kanda nzima ambayo imekumbwa na misukosuko ya kisiasa tangu miaka ya 1990.