Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 18:47

Wa-Algeria waendelea na maandamano licha ya kuchaguliwa rais wa muda


Polisi watumia mabomba ya maji kuwatawanya waandamanaji mjini Algiers
Polisi watumia mabomba ya maji kuwatawanya waandamanaji mjini Algiers

Waandamanaji walikusanyika kwenye uwanja mashuhuri mbele ya jengo la Post kuu mjini Algiers wakidai wanataka mageuzi kamili ya mfumo wa serikali, huku maafisa wa polisi wakitumia mabomba ya maji kujaribu kuwatawanya.

Tangu kuanza malalamiko ya wananchi hadi kujiuzulu kwa Rais wa muda mrefu Abdelazizi Bouteflika wiki 9 zilizopita polisi wamekuwa wakisimama kando na kuwaangalia wakiandamana. Lakini hii leo wameonekana wakikabiliana na waandamanaji na kujaribu kuwatawanya.

Wabunge wa Algeria wapiga kura kumchagua rais wa muda baada ya rais Abdelazizi Bouteflika kujiuzulu
Wabunge wa Algeria wapiga kura kumchagua rais wa muda baada ya rais Abdelazizi Bouteflika kujiuzulu

Maandamano yalitokea muda mfupi tu baada ya wabunge kumchagua spika wa baraza kuu la bunge Abdelkader Bensalah, kuwa rais wa muda baada ya kujiuzulu kwa rais wa muda mrefu Abdelaziz Bouteflika, anayeugua, wiki iliyopita kutokana na maandamano makubwa ya wananchi.

Waandamanaji wa Algeria wataka mageuzi jumla ya kidemokrasia baada ya Bouteflika kujiuzulu
Waandamanaji wa Algeria wataka mageuzi jumla ya kidemokrasia baada ya Bouteflika kujiuzulu

Kulingana na katiba ya Algeria, Bensalah, mwenye umri wa miaka 77 ataongoza nchi kwa mda wa siku 90 zijazo na kutayarisha uchaguzi wa rais katika kipindi hicho.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa Bensalah amesema, " ni lazima tuwachiye wananchi wa Algeria nafasi ya kumchagua rais wanaomtaka kwa haraka iwezekanavyo."


XS
SM
MD
LG