Colombia imeanzisha mpango mpya unaolenga kufuatilia ongezeko la biashara ya madawa ya kulevya kwa kiwango kidogo hasa kati ya vijana wenye umri mdogo.
Rais Ivan Duque amesaini maamuzi ya rais yanayowapa mamlaka maafisa wa polisi kukamata na kuharibu dawa za kulevya zinazopatikana na watu katika sehemu za uma, bila kuwafungulia mashtaka watumiaji wa dawa hizo.
Watakaopatikana na madawa ya kulevya watatozwa faini ya dola 70.
Mahakama za Colombia kwa kawaida hutoza kiwango cha chini cha faini kwa gram 20 za bangi, gram moja ya cocaine na gramu mbili za methaqualone.