Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNCHR limekubali kuunga mkono chombo ambacho kitajumuisha wajumbe wa Burundi na Rwanda ili kujadili swala la wakimbizi wa Burundi walioomba hifadhi nchini Rwanda.
Hii inatokea baada ya Kamishna Mkuu wa UNHCR, Phillippo Grandi alipokutana na Rais Pierre Nkuruziza wa Burundi akianza ziara yake ya Bujumbura siku ya Jumanne, baada ya ziara yake ya Jamhud=ri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda ili kushawishi serikali hizo kuongeza kasi mchakato wa kurejesha wakimbizi nyumbani.
Ziara hii inafanyika huku serikali ya Bujumbura ikiendelea kuituhumu Kigali kuwa inawazuia wakimbizi wa Burundi wanaotaka kurejea kwa hiari. Kamishna mkuu wa UNCHR, Phillippo Grandi amesema akiwa pamoja na rais Burundi Pierre Nkurunziza katika mkutano wa faragha, wameangazia tuhuma hizo na kuazimia kuanza kufikiria uwezekano wa kuanzisha chombo maluum inayojumilisha viongozi wa Rwanda na Burundi ili kuzungumzia swala la wakimbizi .
"Nimemuambia kuwa jana nilizungumza na Rais Kagame na sasa nimeongoea na Nkurunziza, tumekubaliana kujifunza uwezekano wa kuanzisha tume ya mazungumzo na kwamba UNCHR itaunga mkono chombo hicho, ambacho kitarahisisha mazungumzo yanayohusiana na wakimbizi walioomba hifadhi nchini Rwanda, munafahamu kuwa chombo kama hicho kiko upande wa Tanzania, nadhani ni muhimu kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya wakimbizi kupitia mazungumzo."
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kupitia msemaji wake Alain Diomede Nzeeyimana amesema serikali ya Burundi iko tayari kuwatuma wajumbe wake katika tume hiyo ya kujadili kuhusu wakimbizi wa Burundi walioomba hifadhi nchini Rwanda.
Rais wa Burundi amemuhakikishia kuwa wakati wowote mkutano kama huo ukiitishwa, wajumbe kutoka wizara ya mambo ya ndani na maafisa wengine watahudhuria, lakini kusisitiza kwamba watatafuta sehemu nyingine nje ya mataifa hayo mawili ili wakutane na watafute jawabu wa matatizo ya wakimbizi hao.
Burundi pia imekuwa ikilaumu UNCHR kutoa idadi isiyo sahihi ya wakimbizi wa Burundi waliotoroka nchi tangu Burundi kuingia katika mgogoro wa kisiasa mwaka wa 2015.
Kamishna mkuu wa UNCHR amesema watafanya hivi karibuni sensa mpya ya wakimbizi kupitia mfumo wa kompyuta .
"Nimemuelezea rais wa Burundi kuwa si sahili lakini nimekubali kuwa tuko na mpango wa kufanya sensa katika nchi zote zinazowapa hifadhi wakimbizi wa Burundi, tutatumia mfumo wa biometric, serikali inatakiwa kuwa na subra."
Burundi inaorodhesha wakimbizi zaidi ya laki nne waliomba hifadhi katika mataifa jirani kwa mjibu wa takwimu za UNCHR huku nchi ya Rwanda ikidaiwa kuwapa hifadhi elfu zaidi ya tisini na mbili.
Kamishana mkuu wa UNCHR anataraji kuzuru kambi za wakimbizi kutoka Kongo walio katika kambi ya wakimbizi ya Ngozi. Ni maswala ya wakimbizi hao kutoka DRC na hali ya wakimbizi wa Burundi waliomba hifadhi katika mataifa jirani ambayo yameangaziwa katika mikuano wake na rais wa Burundi.