Akizungumza wakati wa mazishi ya watu hao watano ambao miili yao ilipatikana siku ya Jumatatu, naibu gavana wa kaunti hiyo, Omar Maalim, alidai kwamba mashirika ya serikali yalihusika kwa vifo vyao kama njia mojawapo ya kupambana na itikadi kali.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, AP, naibu gavana alisema kuwa mauaji hayo yalitekelezwa na vikosi vya jeshi la Kenya, KDF.
“Tuna habari kwamba watu hawa watano walichukuliwa na jeshi kutoka manyumbani mwao, na kushikiliwa kwa muda mfupi katika kituo cha polisi cha Finno," alisema Maalim.
Kamishna wa kaunti hiyo, Fredrick Shisia, alithibitisha kwa njia ya simu kwamba watano hao walikuwa kati ya watu 11 waliokuwa wamekamatwa.Ijumaa usiku.
AP hata hivyo iliripoti kwamba maafisa wa usalama wa serikali ya Kenya hawakupatikana ili kutoa kauli kuhusiana na tuhuma hizo.