Kenya, ambayo ilikuwa haijatia saini makubaliano kuhusu marufuku hiyo yaliyopitishwa na bunge la Afrika Mashariki, imetangaza rasmi kwamba imefanya hivyo.
Waziri wa Mazingira Kenya, Judy Wakhungu, amesema kwamba makubaliano hayo yataanza kutekelezwa miezi sita baada ya utiaji saini wa mkataba huo, ambao umechapishwa katika gazeti rasmi la serikali, Kenya Gazette.
Mifuko hiyo imetajwa na wataalamu wa mazingira kuwa inachangia pakubwa katika uchafuzi wa mazingira.
Mwezi Novemba mwaka jana, bunge la Afrika Mashariki, lilisitisha mjadala kuhusu mswada wa udhibiti wa matumizi ya plastiki, baada ya wawekezaji kutoka Kenya kupinga vikali hatua hiyo.
Wakati huohuo, Kenya imesema kwamba kupiga marufuku mifuko ya plastiki, kungepelekea kutoweka kwa nafasi nyingi za kazi na uwekezaji wa thamani ya mabilioni ya shilingi.
Tayari Tanzania imepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki, huku Uganda ikitangaza kuwa itakarabati marekabisho ya sheria mwaka wa 2009, kuhusu mazingira, ili kupiga marufuku kabisa mifuko hiyo. Rwanda ilipiga marufuku mifuko hiyo mnamo mwaka wa 2006.