Hatua hiyo imefikiwa na CIA Ijumaa wakati tayari Flynn amekuwa katika mvutano na wenzake katika uongozi wa Trump na jumuiya ya kipelelezi, utata ulioenea baada ya kuwepo taarifa kwamba Flynn alivunja itifaki za kidiplomasia katika mazungumzo yake na Balozi wa Russia nchini Marekani. Kuanzia hivi sasa msaidizi huyo hatoweza kutumikia nafasi hiyo.
Msaidizi huyo wa karibu wa Flynn katika Idara ya Usalama wa Taifa, mkurugenzi wa ngazi ya juu wa Afrika, Robin Townley alijulishwa kukataliwa kwake kushikilia wadhifa huo, vyanzo vya habari vimeelezea.
Hilo limemfanya Townley, ambaye ni afisa wa zamani wa usalama wa jeshi la majini aliyekuwa amepitishwa kufanya kazi nyeti kwa uaminifu wake kwa muda mrefu kuachia wadhifa huo, vyanzo mbali mbali vya habari vimeripoti.