Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:29

Wakongo washtushwa na kifo cha Tshisekedi


Tshisekedi afariki akiwa na umri wa miaka 84
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:59 0:00

Kiongozi wa upinzani wa muda mrefu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Etienne Tshisekedi afariki akiwa na umri wa miaka 84 alipokua mjini Brussels kuonana na madaktari wake.

Msemaji wa chama chake cha UDPS alithibitisha Jumatano kwa Sauti ya Amerika kwamba kiongozi huyo alipimwa na daktari wake, na kueleza kwamba hana matatizo makubwa ya afya, lakini kifo chake kilitokea ghafla muda mfupi baadae.

Wafuasi wake mara moja walikusanyika nyumbani kwake na kwenye makao makuu ya chama cha UDPS, kwa mshangao na masikitiko makubwa. Kuna baadhi wanasema walikuwepo aliposafiri Januari 24 kuelekea Brussels kwa matibabu, na waliona alikuwa na afya yake ingawa ni mtu mzima.

Tshisekedi alianza siasa akiwa na wapigania uhuru wa Kongo kabla ya kuwa waziri katika serikali ya rais wa zamani Mobutu Seseseko, kabla ya kuunda chama cha UDPS, chama cha kwanza cha upinzani huko Zaire mwaka 1982.

Baada ya hapo alichaguliwa mara nne kuwa waziri mkuu chini ya Mobutu katika miaka ya 1990, wakati kiongozi huyo alipojaribu kuanzisha mfumo wa kidemokrasia nchini. Lakini mara hizo zote hakuweza kubaki muda mrefu katika cheo hicho kutokana na kugombana na kiongozi huyo wa utawala wa kimabavu.

Baada ya Mobutu kuondolewa madarakani 2001, kutokana na msaada wa Rwanda na Uganda na vikosi vingine vilivyomleta madarakani Laurent Kabila, Tshisekedi akajikuta tena ni mpinzani mkubwa wa Laurent Kabila na baadae mpinzani mkuu wa mtoto wake Joseph.

Akizungumza na sauti ya amerika mwaka 2011 wakati wa ghasia zilizotokea kupinga uchaguzi wa Joseph Kabila, alipotokea wa pili, Tshisekedi alisema hajaamrisha watu kutumia nguvu kugombania haki zao.

Etienne Tshisekedi, akihutubia mkutano wa upinzani Kinshasa Julai 9 2005.
Etienne Tshisekedi, akihutubia mkutano wa upinzani Kinshasa Julai 9 2005.

Sijajuta hata kidogo ni haki ya wakongo kutetea haki yao na kupigania haki zao kwa njia ya amani. Mimi sijaamrisha wafuasi wangu kutumia silaha bali nimewaambia wakusanyike kwa pamoja kupinga matokeo ya ucahguzi wa dikteta.

Amri ya maandamano makubwa ya upinzani daima yamekuwa yakiongozwa na Tshisekedi, na anasifiwa kwa kuweza kuunganisha upinzani kupinga jaribio la Rais Kabila kubaki madarakani baada ya muda wake kumalizika mwezi Disemba mwaka jana.

Msemaji wa vuguvugu la serikali Henri Mova akizungumza na Sauti ya Amerika anasema taifa limempoteza shujaa.

Taifa limempoteza mwanasiasa mkongwe mashuhuri. Na si upinzani pekee uliompoteza kiongozi wao, bali nchi nzima kwani Tshisekedi ni mtu aliyeanza vita vya kisiasa tangu wakati wa kupigania uhuru na inabidi kutambua kwamba alileta mabadiliko makubwa katika siasa za Kongo. Kwa hivyo tunaweza kusema huu ni mwisho wa enzi muhimu ya siasa za nchi hii.

Mtoto wa Tshisekedi Felix anatajwa huenda akawa waziri mkuu wa utawala wa mpito. Wakongo wameanza kuelezea masikitiko yao na matayarisho yanaanza kuupokea mwili wake kutoka Brussels. Wakuu wa UDPS wanasema uchunguzi unafanyika kuweza kujua nini hasa kiilichosababisha kifo chake.

XS
SM
MD
LG