Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:56

Kanali Azali ashinda uchaguzi wa marudio Comoro


Wapigakura wa Komoro wasubiri kupiga kura katika uchaguzi wa
Wapigakura wa Komoro wasubiri kupiga kura katika uchaguzi wa

Kulingana na matokeo yasiyo rasmi Kanali Assoumani aliweza kupata kura 2 271 dhidi ya 1 308 aliyopata mpinzani wake mgombea wa serikali Mohamed Ali Soilhi. Matokeo hayo hivi sasa yatamwezesha Assoumani kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa duru ya pili ulofanyika April 10, ikiwa mahakama ya katiba itaidhinisha matokeo hayo.

Mahakama ya katiba iliamuru kufanyika kwa uchaguzi huo wa Mai 11 baada ya kugundua kulikua na ghasia na kasoro katika baadhi ya wilaya katika kiswa cha Nzuani wakati wa duru ya pili ya uchaguzi wa rais na kueleza kwamba " wakazi wa huko hawakupewa haki yao ya kikatiba kushiriki katika uchaguzi huo."

Matokeo ya uchaguzi wa Jumatano Mai 11yalitangazwa Alhamisi asubuhi na makamu rais wa tume ya uchaguzi Nadjahe Allaoui baada ya mvutano mkubwa baada ya uchaguzi kati ya wajiumbe wa tume.

Kanali Assoumani aliyekua rais wa Comoro kuanzia 1999 hadi 2006, anatarajiwa kurudi madarakani mara baada ya mahakama ya katiba itakapo idhinisha matokeo yote na ataapishwa hapo May 26, 2016.

XS
SM
MD
LG