Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 10:37

Mjadala Waendelea Marekani Kuhusu Wakimbizi wa Syria na Iraq


Mgombea Urais ndani ya chama cha Republikan Ted Cruz.
Mgombea Urais ndani ya chama cha Republikan Ted Cruz.

Mjadala kuhusu kuwakubali wakimbizi wa Syria umeibuka upya katika bunge la Marekani na kufanyika mikutano na wanahabari iliyokuwa na maoni tofauti.

Maoni hayo yalielemea namna ya kuifanya Marekani kuwa salama na kuendeleza desturi za Kimarekani katika kushughulikia shauri hilo.

Seneta wa chama cha Republikan na mgombea wa urais Ted Cruz ametangaza sheria ya kuzuia wakimbizi kutoka Syria na kuruhusu majimbo kuchagua kuwapokea wakimbizi wanaotoka maeneo yanayoshikiliwa na kundi la Islamic State.

“Hapa anasema tuna amiri jeshi mkuu ambaye anakataa kukiri kuna adui, wala kumkemea, hata kufanya machache kwa yale yanayoweza kumshinda adui. Kama Rais Obama hataongoza, basi ni juu ya wa-Republikan na wademokrat ndani ya Bunge kusimama kidete." Alisema Cruz

Wakati huohuo, Seneta Patrick Leahy na Wademokrat wengine walikusanyika na viongozi wa kiroho kwa tukio lao wenyewe.

Katika mkutano wao Leah alisema “ inashitusha kusikia wote wanaosema funga milango kwenye mipaka yetu. Kama tukijibu kwa kufunga mlango, tunachokifanya ni kutoa msaada kwa adui zetu.”

Seneta Tim Kaine alisimama mbele ya picha ya mtoto wa kiume wa Syria ambaye alipoteza maisha katika ufukwe wa Uturuki mapema mwaka huu.

“Wakimbizi si maadui zetu. Wanawakimbia adui zetu. Tumewapa jina la maadui wale wote wanaohitaji msaada wetu.” Alisema bwana Kaine

Rais Barack Obama ameahidi kutumia kura yake ya turufu kwa muswada wowote utakao kataa Marekani kuwakubali wakimbizi kutoka Syria au Iraq.

Mwezi uliopita, baraza la wawakilishi lilipiga kura kufanya hivyo lakini haiko wazi kama lini Seneti watauchukua muswada huo ama ule unaofanana.

XS
SM
MD
LG