Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 19:13

Al-Shabab yadai kuwajibika na shambulio la Garissa Kenya


Wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa wanajificha ndani ya gari baada ya kukimbia kutoka shambulizi la chuo chao Garissa, Kenya, April 2, 2015.
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa wanajificha ndani ya gari baada ya kukimbia kutoka shambulizi la chuo chao Garissa, Kenya, April 2, 2015.

Kundi la wanamgambo wa Kisomali la Al-Shabab limedai kuwajibika na shambulio katika chuo kikuu cha Garissa kilichopo kaskazini- mashariki ya Kenya, na kusababisha vifo vya watu 147.

Kufuatana na mwandishi wa habari wa Sauti ya Amerika-VOA mjini Garissa, watu 65 wamejeruhiwa na idadi isiyojulikana ya wanafunzi wanashikiliwa mateka na karibu wanafunzi wengine 400 hawajulikani mahala walipo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:58 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Msemaji wa kundi hilo lenya uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda, Sheikh Ali Mohamed Rage, aliliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP kwamba wanamgambo wao walishambulia chuo kikuu hicho Alhamisi alfajiri na kuwachukua mateka wanafunzi wote wakristo na kuwaachilia huru waislamu.

Milio ya bunduki ya hapa na pale imekuwa ikisikika saa sita baada ya shambulio hilo, wakati wizara ya mambo ya ndani ya Kenya ikiripoti kwamba washambulizi wamezingirwa katika eneo moja.

Rais Uhuru Kenyatta alilihutubia taifa kueleza kitendo hicho cha Garissa akitoa rambi rambi zake kwa familia za walioathiriwa na kuwahakikishia wananchi kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika na shambulio hilo.

XS
SM
MD
LG