Hatua hiyo inadhihirisha kuimarika kwa taifa hilo la Afrika Mashariki katika kutegemea mikopo ya China baada ya Benki ya Dunia kusitisha misaada yake kwa nchi hiyo kutokana na sheria kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
Wizara ya Fedha na wizara ya habari waliiomba Bunge kuidhinisha serikali kuomba mkopo huo kutoka Uchina.
Kulingana na wizara ya fedha, fedha hizo zitatumika katika kufadhili miradi ya serikali, uwekaji, uagizaji na usaidizi wa miundombinu ya kitaifa.
Aidha Uganda iko kwenye mazungumzo na wakala wa mikopo wa mauzo ya nje wa China SINOSURE na Benki ya Exim kwa mkopo wa kufadhili ujenzi wa bomba la kusaidia Uganda kuuza nje mafuta yake ghafi katika masoko ya kimataifa.
Benki ya Dunia, ambayo kwa kawaida ni mkopeshaji mkuu wa maendeleo wa Uganda, ilisitisha mikopo kwa Uganda baada ya Rais Yoweri Museveni kutia saini Sheria ya Kupinga Mapenzi ya jinsia moja ambayo inatoa hukumu kali ikiwa ni pamoja na kifo.
Forum