Mgombea anayaetarajiwa kuwa mteule wa urais wa kupitia chama cha Republican Donald Trump anasema akichaguliwa atarejesha tena marufuku ya kusafiri kwa baadhi ya nchi zenye waislamu wengi katika siku ya kwanza ya utawala wake mpya.
Mahakama moja inayoungwa mkono kimataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati siku ya Jumanne ilitoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, aliye uhamishoni, François Bozize, kwa ukiukaji wa haki za binadamu kuanzia mwaka 2009 hadi 2013, msemaji wao alisema.
Betri zimekuwa muhimu katika ongezeko la magari ya umeme lakini pia ni muhimu kwa nishati ya upepo na jua.
Waziri Blinken pia alijadili juhudi za kidiplomasia zinazoendelea ili kufikia amani ya kudumu katika eneo la Gaza
Gavana Oleh Kiper alisema shambulio hilo la Russia lilipiga moja ya maeneo maarufu mjini Odesa ambapo watalii huenda kutembea
Mvua zimesababisha vifo vya watu takriban 170 na wengine 185,000 kukoseshwa makazi tangu mwezi Machi, ofisi ya rais imesema.
Picha za video ziliwaonyesha waandamanaji katika chuo cha Manhattan cha Columbia walifunga mikono mbele ya ukumbi wa Hamilton.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema Jumatatu nchi yake inashughulikia kuongeza uwezo wake wa ndege zisizo na rubani - drones, wakati nchi hiyo ikipambana kuzima uvamizi wa Russia ulioanza zaidi ya miaka miwili iliyopita.
Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken amewasili Riyadh kwa ajili ya mazungumzo ya kikanda Jumatatu na Jumanne kuhusu msaada wa kibinadamu huko Gaza, mpango baada ya vita kwa maeneo ya Palestina, na utulivu na usalama katika Mashariki ya Kati.
Wapiganaji wanaoshukiwa wa ISWAP walitumia kifaa cha milipuko kulipua gari lililowabeba Civilian Joint Task Force
Watu katika mitaa ya pembeni mwa mji mkuu Lome waligawanyika juu ya uchaguzi na nani anapaswa kuongoza.
HRW imeyataja mauaji hayo miongoni mwa matukio mabaya ya unyanyasaji unaofanywa na jeshi la Burkina Faso tangu 2015
Pandisha zaidi