Njaa na Utapiamlo unaenea kote nchini Sudan, mwaka moja tangu kuzuka kwa vita kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha dharura cha (RSF) huku ikiwa hakuna dalili ya vita kusitishwa hivi karibuni.
Jeshi la Marekani linapanga kurejea Chad ndani ya mwezi mmoja kwa ajili ya mazungumzo kuhusu kurekebisha makubaliano ambayo yanairuhusu kubakisha wanajeshi huko, jenerali mmoja wa Marekani alisema Jumatano.
Mwaka huu Sherehe za Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi zina hisia ya dharura ya kujitolea upya kwa haki za kijamii, wakati tunapopitia kipindi kigumu, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa na mabadiliko ya haraka katika sehemu za kazi kutokana na maendeleo ya teknolojia.
Mahakama moja inayoungwa mkono kimataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati siku ya Jumanne ilitoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, aliye uhamishoni, François Bozize, kwa ukiukaji wa haki za binadamu kuanzia mwaka 2009 hadi 2013, msemaji wao alisema.
Kamanda mkuu wa kundi la Islamic State aliyekuwa akitafutwa kwa kuhusiana na vifo vya wanajeshi wa Marekani huko Niger wameuawa katika operesheni ilikuwa ikiendeshwa huko na wanajeshi wa Mali, jeshi la nchi hiyo limesema.
Betri zimekuwa muhimu katika ongezeko la magari ya umeme lakini pia ni muhimu kwa nishati ya upepo na jua.
Waziri Blinken pia alijadili juhudi za kidiplomasia zinazoendelea ili kufikia amani ya kudumu katika eneo la Gaza
Gavana Oleh Kiper alisema shambulio hilo la Russia lilipiga moja ya maeneo maarufu mjini Odesa ambapo watalii huenda kutembea
Mvua zimesababisha vifo vya watu takriban 170 na wengine 185,000 kukoseshwa makazi tangu mwezi Machi, ofisi ya rais imesema.
Picha za video ziliwaonyesha waandamanaji katika chuo cha Manhattan cha Columbia walifunga mikono mbele ya ukumbi wa Hamilton.
Mahakama kuu nchini Ghana imefuta mashitaka kwa Rais Nana Akufo-Addo ya kushindwa kuchukua hatua za haraka kuhusiana na mswaada unaopinga Ushoga (LGBTQ) iliyopitishwa na Bunge mwezi Februari, ilitua hukumu hiyo Jumatatu.
Umoja wa Ulaya umeamua kuweka masharti makali ya visa kwa raia wa Ethiopia kwa ukosefu wa ushirikiano kutoka kwa serikali ya Ethiopia juu ya kurudishwa nyumbani kwa wale wanaokaa kinyume cha sheria, baraza la EU limesema siku ya Jumatatu.
Pandisha zaidi