Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 07:07

Korea Kaskazini yafunga balozi za nchi nne zikiwemo Uganda na Angola


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un (katikati) akizungumza na viongozi wa Russia huko Primorsky, Septemba 17,20023. Picha na KCNA KUPITIA KNS / AFP.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un (katikati) akizungumza na viongozi wa Russia huko Primorsky, Septemba 17,20023. Picha na KCNA KUPITIA KNS / AFP.

Korea Kaskazini imeamua kufunga ofisiza kibalozi katika angalau mataifa manne duniani kote, mabadiliko makubwa ya kidiplomasia ambayo baadhi ya wachambuzi wanasema yanaweza kuashiria changamoto kubwa za kiuchumi.

Kulingana na msururu wa ripoti za vyombo vya habari zilizoanza kuibuka wiki iliyopita, Korea Kaskazini itafunga balozi zake nchini Uganda, Angola na Uhispania, pamoja na ubalozi wake mdogo huko Hong Kong.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini siku ya Ijumaa ilithibitisha idadi isiyojulikana ya balozi zilizofungwa, ikikariri "mabadiliko katika mazingira ya kimataifa na sera ya serikali ya mambo ya nje."

"Uhamishaji mzuri na uendeshaji wa jeshi la kidiplomasia la serikali ni sehemu ya shughuli za kawaida zinazofanywa na mataifa huru kwa nia ya kukuza maslahi yao ya kitaifa katika uhusiano wa nje," ilisema taarifa hiyo iliyoko kwenye tovuti ya wizara hiyo.

Taarifa ya Korea Kaskazini pia ilisema kuwa balozi mpya zitafunguliwa lakini haikutoa maelezo zaidi.

Wizara ya Muungano ya Korea Kusini, ambayo inashughulikia uhusiano na Korea Kaskazini, imetaja kufungwa kwa balozi hizo kunatokana na kuongezeka kwa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Korea Kaskazini, ambavyo vimetatiza shughuli za upataji fedha kwa ajili ya balozi zake nchi za nje ya nchi.

"Hii ni moja ya suala ambalo linaonyesha hali ngumu ya kiuchumi ya Korea Kaskazini, ambapo sasa ni vigumu hata kudumisha uhusiano mdogo wa kidiplomasia na nchi ambazo ni marafiki wa asili," afisa wa Korea Kusini aliviambia vyombo vya habari vya ndani.

Kabla ya kufungwa, Korea Kaskazini ilikuwa na ofisi za kibalozi katika maeneo 53, kulingana na wizara ya muungano ya Korea Kusini.

Balozi nyingi za Korea Kaskazini zimehusika katika ulanguzi wa silaha, dawa, na bidhaa za anasa, pamoja na shughuli nyingine haramu za kibiashara zilizokusudiwa kupata pesa taslimu kwa serikali yao iliyotengwa kiuchumi, kulingana na ripoti za vyombo vya habari

Forum

XS
SM
MD
LG