Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ameelezea imani yake kwamba Russia inaweza kushindwa na kuonya kuwa vita nchini Ukraine vimeonyesha kuwa Ulaya inapaswa kuendeleza utengenezaji wa silaha za pamoja na Ukraine na kujenga silaha za kutosha kwa ajili ya ulinzi wake.
Miaka miwili ya vita hivi imethibitisha kwamba Ulaya inahitaji silaha zake za kutosha kwa ajili ya ulinzi wa uhuru. uwezo wake ili kujihakikishia ulinzi. Uwezo wake wenyewe ambao utairuhusu Ulaya yote, au sehemu yoyote, kusimama na kujihifadhi chini ya hali yoyote ya ulimwengu, alisema Zelensky.
Zelenskyy alitoa matamshi hayo kupitia video katika mkutano wa masuala ya ulinzi wa Stockholm Jumapili, wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden, Tobias Billstrom alielezea kujitolea kwa nchi yake kuiunga mkono Kyiv. Msaada wa kijeshi, kisiasa, na kiuchumi kwa Ukraine unabaki kuwa jukuu kuu katika sera ya mambo ya nje ya serikali ya Sweden kwa miaka ijayo, alituma ujumbe kwenye mtandao wa X, zamani Twitter, wakati mkutano unaendelea.
Japan pia imeahidi kuiunga mkono Kyiv Jumapili wakati waziri wa mambo ya nje wa Japan, Yoko Kamikawa alipofanya ziara ambayo haikutangazwa, na kuwa mgeni wa kwanza rasmi wa kigeni katika mji mkuu wa Ukraine mwaka 2024.