Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ameshangiliwa sana katika Chuo Kikuu cha Ulinzi wa Taifa mjini Washington siku ya Jumatatu baada ya kuwahutubia maafisa wa jeshi la Marekani, akianza ziara yake mjini Washington kwa lengo la kulishawishi Bunge kutoa msaada zaidi wa kijeshi kwa Ukraine kabla ya ufadhili kwisha.
Katika hotuba yake, Zelenskyy alisisitiza umuhimu wa kuishinda Russia nchini Ukraine kwa sababu alisema, ikiwa Russia itaishinda Ukraine, Rais wa Russia Vladimir Putin hatoishia hapo. Silaha yake Putin dhidi yetu kwa sasa ni propaganda na taarifa za uongo. Lakini kama ataona fursa, atakwenda mbali zaidi, alisema. Hivi sasa anaubadilisha uchumi wa Russia na jamii juu ya kile anachokiita “njia za vita”.
Zelenskyy alisema uhuru lazima ushinde pale unapopata changamoto na aliwashukuru Wa-Marekani kwa msaada huo.