Zelensky aapa hawatasimama hadi watakapoikomboa Ukraine yote

Rais wa Ukraine Zelenskiy akihutubia wananchi wa Ukraine kuhusu kubadilishana wafungwa wa vita (POWs), mjini Kyiv. September 22, 2022. REUTERS.

Rais wa Ukraine alielezea kwa kina kesi dhidi ya uvamizi wa Russia katika Umoja wa Mataifa na aliomba adhabu kutoka kwa viongozi wa dunia katika hotuba yake Umoja wa Mataifa.

Rais wa Ukraine alielezea kwa kina kesi dhidi ya uvamizi wa Russia katika Umoja wa Mataifa na aliomba adhabu kutoka kwa viongozi wa dunia katika hotuba yake Umoja wa Mataifa.

Hotuba hiyo iliyotolewa saa chache baada ya Moscow kutoa tangazo la kipekee kwamba itawaandikisha baadhi ya wanajeshi wa akiba kwa ajili ya vita nchini Ukraine.

Akiwa amepata nguvu kutokana na mashambulizi ambayo yamewawezesha wanajeshi wake kukomboa tena maeneo ambayo Wa-Russia waliyakamata, Volodymyr Zelensky aliapa katika hotuba yake kwa njia ya video siku ya Jumatano kwamba wanajeshi wake hawatasimama hadi watakapoikomboa Ukraine yote.

"Tunaweza kurudisha bendera ya Ukraine katika ardhi yetu kamili. Tunaweza kufanya hivyo kwa nguvu ya silaha," rais alisema katika hotuba iliyotolewa kwa Kiingereza. "Lakini tunahitaji muda."

Hotuba za video za Zelensky akiwa amevalia fulana ya kijani kibichi zimekuwa jambo la kawaida. Lakini hotuba hii ilikuwa moja ya hotuba iliyotarajiwa sana katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambako vita vimetawala.